‘Mtu mmoja hufa kila baada ya saa sita’

Muktasari:

Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Mathias Nyange alisema hayo jana kwenye kikao cha majumuisho ya Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Chiku Galawa baada ya kumaliza kutembelea halmashauri zote.

Vwawa. Mtu mmoja hufariki dunia kila baada ya saa sita mkoani Songwe kutokana na imani za kishirikina.

Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Mathias Nyange alisema hayo jana kwenye kikao cha majumuisho ya Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Chiku Galawa baada ya kumaliza kutembelea halmashauri zote.

Nyange alisema imani potofu ni chanzo cha mauaji hayo yanayokana na baadhi ya waganga wa jadi wanaoendelea kupiga ramli chonganishi.

Mkuu wa mkoa, Galawa alisema changamoto nyingi zinakwamisha juhudi za kuwaletea maendeleo wananchi na kuagiza halmashauri zijipange kutatua kero hiyo ya mauaji.