NHC yaeleza kwa nini nyumba zake ni ghali

Meneja masoko wa shirika la Nyumba la Taifa ,Erasto Chilambo

Muktasari:

  • Akizungumza na wanahabari mapema leo Jumanne, meneja masoko wa shirika hilo, Erasto Chilambo amesema endapo shirika hilo lingekuwa linasaidiwa ardhi bei ya nyumba ingekua nafuu sana.

Dar es Salaam. Shirika la Nyumba la Taifa(NHC) limesema gharama za ardhi kwaajili ya ujenzi wa nyumba zake inachangia kwa kiasi kikubwa nyumba hizo kuuzwa kwa bei ya juu.

Akizungumza na wanahabari mapema leo Jumanne, meneja masoko wa shirika hilo, Erasto Chilambo amesema endapo shirika hilo lingekuwa linasaidiwa ardhi bei ya nyumba ingekua nafuu sana.

"Bei ya chini ya nyumba ni milion 34 ambayo ingeweza kushuka zaidi hata kufika milion 20 na... kwa nyumba moja," amesema.