‘Ng’ombe waliokatwa mkia’ wazua mjadala

Aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida, Mgana Msindai.

Muktasari:

  • Katika mkutano huo uliofanyika mjini Dodoma Jumamosi iliyopita, baadhi ya makada akiwamo aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida, Mgana Msindai na Fred Mpendazoe walitangaza kurejea kwenye chama hicho.

Dar es Salaam. Hatua ya baadhi ya makada waliokuwa vyama vya upinzani kurudi CCM na kauli ya Mwenyekiti mpya wa chama hicho, Rais John Magufuli kuwafananisha na ng’ombe aliyekatwa mkia, imezua mjadala huku wenyewe wakitetea uamuzi wao wa kurudi.

Katika mkutano huo uliofanyika mjini Dodoma Jumamosi iliyopita, baadhi ya makada akiwamo aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida, Mgana Msindai na Fred Mpendazoe walitangaza kurejea kwenye chama hicho.

Akizungumzia kauli ya Rais Magufuli, kada wa zamani wa CCM, Njelu Kasaka alisema inaashiria kuwa chama hicho hakina imani tena na makada wanaorejea. 

Hata hivyo, Mpendazoe alisema wapinzani hawana dhamira ya kweli ya kuleta mabadiliko wanayohubiri.