Safari ya miaka 43 kutimia Septemba

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa

Muktasari:

  • Majaliwa alikuwa anatekeleza uamuzi wa Rais John Magufuli alioubainisha wakati anakabidhiwa kijiti cha uenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na kuusisitiza jana kwenye Maadhimisho ya Siku Mashujaa.

Dodoma/Dar. Safari ya Serikali ya kuhamia Dodoma imeiva na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amejipa mwezi mmoja akisema atakuwa tayari kuhama Septemba.

Majaliwa alikuwa anatekeleza uamuzi wa Rais John Magufuli alioubainisha wakati anakabidhiwa kijiti cha uenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na kuusisitiza jana kwenye Maadhimisho ya Siku Mashujaa.

Akizungumza katika maadhimisho hayo, Majaliwa aliwaita wasaidizi wake na kuwataka kukamilisha nyumba yake iliyopo eneo la Mlimwa ili aweze kuhamia.

Alitoa maagizo hayo kwa Waziri wa Nchi (Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu), Jenista Mhagama na katibu mkuu wa ofisi yake akisema ahadi ya kuhamia Dodoma ilitolewa na Rais wa Kwanza wa Tanzania, Mwalimu Julius Nyerere na Dk John Magufuli wakati wa kampeni zake mwaka jana na kinachofanyika sasa ni utekelezaji.