Tasaf yajipanga kupunguza kiwango cha umasikini

Mkurugenzi wa kujenga uwezo wa Tasaf, Amadeus Kamagenge amesema matarajio mengine ni kupunguza pengo la umasikini kwa asilimia 43.

Muktasari:

  • Akizungumza wakati akitoa taarifa kwa Kamati ya Baraza la Wawakilishi ya kusimamia ofisi za viongozi wakuu wa baraza hilo mkurugenzi wa kujenga uwezo wa Tasaf, Amadeus Kamagenge alisema matarajio mengine ni kupunguza pengo la umasikini kwa asilimia 43.

Dar es Salaam. Imeelezwa kuwa mafanikio yanayotarajiwa kwenye mpango wa tatu wa utekeleza wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (Tasaf) ni kupunguza kiwango cha umasikini uliokithiri kwa asilimia 52.

Akizungumza wakati akitoa taarifa kwa Kamati ya Baraza la Wawakilishi ya kusimamia ofisi za viongozi wakuu wa baraza hilo mkurugenzi wa kujenga uwezo wa Tasaf, Amadeus Kamagenge alisema matarajio mengine ni kupunguza pengo la umasikini kwa asilimia 43.

Alisema kuongezeka kwa kipato cha kaya na kuweza kushiriki katika kuweka akiba na kuwekeza katika shughuli za maendeleo.

"Miongoni mwa mafanikio ya awamu mbili zilizotangulia ni pamoja na kutoa elimu kwa jamii ya kupunguza umasikini na kupambana na utapiamlo, matarajio ya awamu hii ni kufika mbali zaidi.”