Thursday, April 20, 2017

Ten-Met yaandaa maadhimisho ya elimu

 

By Prosper Kaijage, Mwananchi Pkaijage@mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mtandao wa Elimu Tanzania (Ten-Met)  umeandaa maadhimisho ya wiki ya uhamasishaji wa elimu bora nchini. 

Hayo yamesemwa leo (alhamisi) na Mratibu wa TenMet, Cathleen Semkwao alipozungumza na waandishi wa habari.

Semkwao alisema  maadhimisho hayo yatafanyika Mtwara wilaya ya Nanyumbu kuanzia tarehe 24-28 mwezi huu. 

Amesema lengo la Maadhimisho hayo ni kuhamasisha jamii na wadau wengine kutoa mwanya wa mtu kupata elimu bora na yenye tija.

Kauli mbiu ya maadhimisho hayo mwaka huu kidunia ni "uwajibikaji wa pamoja kwa Elimu bora na jumuishi" amesema Sekwao.

-->