Wakulima Moshi washauriwa kuongeza thamani ya kahawa

Muktasari:

  • Akizungumza wakati wa mafunzo ya namna ya kutengeneza kahawa kwa kutumia mashine ya expesso, Mwenyekiti wa Chama cha Wanawake Wahamasishaji Kilimo cha  Kahawa Tanzania (Tawoca),  Fatma Faraji alisema wanawake hawanufaiki na zao hilo licha ya kuwa wanaliza zaidi kuliko wanaume.

Moshi. Imeelezwa kuwa asilimia 80 ya wanawake mkoani Kilimanjaro hawanufaiki na kilimo cha kahawa kutokana na kushindwa kusindika zao hilo na kuongeza thamani.

Akizungumza wakati wa mafunzo ya namna ya kutengeneza kahawa kwa kutumia mashine ya expesso, Mwenyekiti wa Chama cha Wanawake Wahamasishaji Kilimo cha  Kahawa Tanzania (Tawoca),  Fatma Faraji alisema wanawake hawanufaiki na zao hilo licha ya kuwa wanaliza zaidi kuliko wanaume.

Wadau wa kahawa mkoani Kilimanjaro wametakiwa kuelimisha wanawake kulima zao hilo kwa wingi na kujihusisha katiak mnyororo wa thamani, kutokana na kuwa wazalishaji mahiri kuliko wanaume.

Makamu Mwenyekiti wa Tawoca, Ida Makamba alisema ni vyema wanawake wanaolima kahawa kutouza yote, badala yake wafungue migahawa.

Mratibu wa Kahawa Wilaya ya Moshi, Violeth Kisanga alisema katika kuhamasisha wanawake kulima zao hilo, wameanzisha zaidi ya vikundi 200 vya wanawake wa mikoa ambayo inajihusisha na kilimo hicho.