Wanaodaiwa kufungua akaunti feki ya maafa wasomewa mashtaka

Muktasari:

  • Watuhumiwa hao ni pamoja na Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera, Amantius Msole, Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Bukoba,Steven Makonda na Mhasibu wa Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba,  Simbaufoo Swai.
  • Walisomewa mashtaka ya kula njama na kufungua akaunti feki na kutumia vibaya madaraka vyao.

Vigogo watatu wanaotuhumiwa kufungua akaunti feki yenye jina la ‘Kamati ya Maafa kagera’ kwa ajili ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu, wamesomewa mashtaka katika mahakama ya Hakimu Mkazi, Bukoba leo.

 Watuhumiwa hao ni pamoja na Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera, Amantius Msole, Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Bukoba,Steven Makonda na Mhasibu wa Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba,  Simbaufoo Swai.

 Walisomewa mashtaka ya kula njama na kufungua akaunti feki na kutumia vibaya madaraka vyao.

Watuhumiwa hao walisimamishwa kazi juzi kwa kosa la kufungua akaunti feki yenye jina kama linalotumiwa na akaunti ya serikali  kwa ajili ya kupokea misaada ya waathirika wa maafa ya Kagera ‘Kamati ya Maafa Kagera’