Watanzania waombwa kujitokeza Fahamu Talk

Mhamasishaji Ujasiriamali, Anthony Luvanda akizungumza na waandishi Dar es Salaam kuhusu kongamano la Fahamu  Talk litakalofanyika  katika Ukumbi wa Nkurumah wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam  Jumapili ijayo. Picha na Salim Shao

Muktasari:

  • Mbali na hilo, katika Fahamu Talk ambayo inadhaminiwa na wadau mbalimbali likiwemo gazeti la Mwananchi, wananchi pia watajifunza masuala ya mahusiano ambayo kwa namna moja yamekuwa wakichangia kurudisha nyuma juhudi za watu mbalimbali katika kujikwamua kiuchumi.

Dar es Salaam.   Watanzania wametakiwa kujitokeza kushiriki katika kongamano la Fahamu Talk litakalofanyika Septemba 4 mwaka huu, katika ukumbi wa Nkuruma, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), kwa ajili ya kupata fursa ya kujifunza masuala mbalimbali  hasa yale yatakayo wawezesha kuimarisha uchumi binafsi.

Mbali na hilo, katika Fahamu Talk ambayo inadhaminiwa na wadau mbalimbali likiwemo gazeti la Mwananchi, wananchi pia watajifunza masuala ya mahusiano ambayo kwa namna moja yamekuwa wakichangia kurudisha nyuma juhudi za watu mbalimbali katika kujikwamua kiuchumi.

Mtaalamu wa saikolojia na mahusiano, Dk Chris Mauki pamoja na mjasiriamali, Anthony Luvanda ambao watakuwa wazungumzaji kwenye Fahamu Talk, wamesema hiyo ni fursa ya pekee kwa wananchi kujifunza masuala hayo ili waweze kuboresha mahusano yao katika maeneo mbalimbali wanapofanya shughuli zao na mwisho wa siku kuimarisha uchumi wao.

Hata walisema ili mtu aweze kushiriki atatakiwa kuchangia Sh20,000 kwa ajili ya chakula na vinywaji vya  siku hiyo.