Wavunaji wa mkaa sasa watumia baiskeli, pikipiki

Muktasari:

  • Akizungumza na waandishi wa habari leo mkuu wa kitengo cha mawasiliano Glory Mziray alisema mkaa ndio kichocheo kikubwa cha uharibifu wa misitu kutokana na kuvunwa na kusafirishwa kinyume cha sheria na taratibu.

Dar es Salaam. Wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS) inaendelea na mkati wa kuimarisha utekelezaji wa Sheria ya Misitu kwenye masuala ya usimamizi,uvunaji na usafirishaji wa mazao ya misitu hususan mkaa.

Akizungumza na waandishi wa habari leo mkuu wa kitengo cha mawasiliano Glory Mziray alisema mkaa ndio kichocheo kikubwa cha uharibifu wa misitu kutokana na kuvunwa na kusafirishwa kinyume cha sheria na taratibu.

"Kwa miaka ya karibuni kumekuwa na ongezeko kwa wavunaji kusafirisha mkaa,nguzo,kuni na vipande vya magogo kwa kutumia pikipiki na baiskeli" alisema Mziray