15 watiwa mbaroni kwa uhalifu Moshi

Kamanda wa Polisi mkoani hapa,Wilbrod Mutafungwa.

Muktasari:

Polisi mkoani Kilimanjaro imewakamata watu 15 wakiwamo askari polisi wawili waliofukuzwa kazi, wakituhumiwa kwa vitendo vya uhalifu ikiwamo ujambazi wa kutumia silaha na biashara ya dawa za kulevya.

Moshi. Polisi mkoani Kilimanjaro imewakamata watu 15 wakiwamo askari polisi wawili waliofukuzwa kazi, wakituhumiwa kwa vitendo vya uhalifu ikiwamo ujambazi wa kutumia silaha na biashara ya dawa za kulevya.

Kamanda wa Polisi mkoani hapa,Wilbrod Mutafungwa amesema watuhumiwa hao wanashikiliwa kwa makosa tofauti yakiwamo ya kujihusisha na ujambazi na kukutwa na dawa za kulevya za aina tofauti.

Pia, Mutafungwa amesema raia wa Kenya, Edward Gaithuru (53) na Chrispin Mecharia wakazi wa Nairobi wanashikiliwa kwa tuhuma za kuwatapeli wateja wanaotoa na kuweka fedha zao benki.