15 wauawa, 45 wajeruhiwa baada ya shambulio la kisu

Picha ya AFP.

Muktasari:

  • Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na   Shirika la Utangazaji la Japan NHK, mtuhumiwa wa shambulio hilo anashikiliwa na Jeshi la polisi la nchini humo.
  • Mtuhumiwa huyo mwenye umri wa miaka 26, alikamatwa na Polisi akiwa katika jaribio la kujiua.

Tokyo.  Watu 15 wameuawa na 45 kujeruhiwa baada ya mtu mmoja kuvamia kituo cha walemavu cha Samihara nje kidogo ya jiji la Tokyo na kufanya shambulio la kisu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na   Shirika la Utangazaji la Japan NHK, mtuhumiwa wa shambulio hilo anashikiliwa na Jeshi la polisi la nchini humo.

Mtuhumiwa huyo mwenye umri wa miaka 26, alikamatwa na Polisi akiwa katika jaribio la kujiua.

Vituo kadhaa vya televisheni nchini Japani vimekuwa vikionyesha idadi kubwa ya magari ya wagonjwa yakibeba wagonjwa kutoka kwenye eneo la tukio na kuwakimbiza kwenye hospitali ya jirani.

Taarifa za awali zilizotolewa na Shirika la habari la Kyodo zilieleza kuwa watu 19 walifariki na 20 kujeruhiwa taarifa ambayo baadaye ilisahihishwa.