Lowassa ‘ageuzwa ajenda’ CCM

Muktasari:

Jinamizi hilo lilionekana kutawala ndani ya ukumbi huo huku kila aliyepewa nafasi ya kuzungumza akionyesha wazi kutaja kundi lililoongozwa na waziri huyo mkuu wa zamani, ambaye alijiondoa CCM baada ya jina lake kukatwa kwenye mbio za urais na Chadema.

Dodoma. Mzimu wa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa jana ulitawala Mkutano Mkuu Maalumu wa chama hicho uliofanyika Ukumbi wa CCM Convention Center eneo la Makuru mjini hapa.

Jinamizi hilo lilionekana kutawala ndani ya ukumbi huo huku kila aliyepewa nafasi ya kuzungumza akionyesha wazi kutaja kundi lililoongozwa na waziri huyo mkuu wa zamani, ambaye alijiondoa CCM baada ya jina lake kukatwa kwenye mbio za urais na Chadema.

Mwenyekiti aliyemaliza muda wake, Jakaya Kikwete ndiye aliyekuwa wa kwanza kuzungumzia hali ya mchakato huo kuwa ulikuwa mgumu na majaribu makubwa na kwamba wazee walifanya kazi kubwa kunusuru hali.