Chadema ‘wamweka mezani’ Rais Magufuli

Muktasari:

Tofauti na ilivyozoeleka, jana Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe hakutoa hotuba ya ufunguzi na kuwataka wanahabari kusubiri maazimio aliyodai yatatolewa baada ya kumalizika kwa kikao hicho cha siku mbili kinachofanyika Hoteli ya Ledger Plaza Bahari Beach.

Dar es Salaam. Wakati wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM wakimchagua kwa kishindo Rais John Magufuli kuwa mwenyekiti mpya wa chama hicho jana mjini Dodoma, Chadema kilifanya kikao cha Kamati Kuu kujadili mambo 16 kilichosema yanafanyika ‘ovyo’ tangu mkuu huyo wa nchi aingie madarakani, Novemba 5, mwaka jana.

Tofauti na ilivyozoeleka, jana Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe hakutoa hotuba ya ufunguzi na kuwataka wanahabari kusubiri maazimio aliyodai yatatolewa baada ya kumalizika kwa kikao hicho cha siku mbili kinachofanyika Hoteli ya Ledger Plaza Bahari Beach.

Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano, Uenezi na Mambo ya Nje wa chama hicho, John Mrema ndiye aliyepewa jukumu la ‘kuwapoza’ wanahabari na kusisitiza kuwa kikao hicho kinajadili mambo mazito, ambayo ni vyema wakubaliane kwanza.