Bodaboda elimu yaanza kuwaingia

Muktasari:

Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Awadh Haji alisema juzi kuwa baada ya operesheni hiyo endelevu baadhi ya waendesha pikipiki wanafuata sheria.

Dar es Salaam. Ajali za pikipiki zimepungua kwa asilimia 80 jijini Dar es Salaam, baada ya polisi kufanya  operesheni kuhakikisha madereva wanafuata sheria.

Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Awadh Haji alisema juzi kuwa baada ya operesheni hiyo endelevu baadhi ya waendesha pikipiki wanafuata sheria.

Haji alisema bodaboda wanatakiwa kuwa na leseni ya kuendesha pikipiki, kuvaa kofia ngumu ‘helmet’ na kuacha kupandisha mishikaki.

Mwendesha pikipiki, Nitha Mchia alisema ajali zimepungua kutokana na elimu wanayopewa na mafunzo ya mara kwa mara.