Mrema, Cheyo wasalimu kwa CCM

Muktasari:

Wakizungumza kwenye mkutano huo, Mwenyekiti wa TLP, Augustine Mrema alisema anavishangaa vyama vingine vya upinzani kususia vikao vya Bunge.

Dodoma. Baadhi ya vyama vya upinzani vilivyohudhuria Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM, vimevikandia vyama vingine vya upinzani vikeleza kuwa hakuna kama CCM kwani kigumu kung’olewa madarakani.

Wakizungumza kwenye mkutano huo, Mwenyekiti wa TLP, Augustine Mrema alisema anavishangaa vyama vingine vya upinzani kususia vikao vya Bunge.

“Rais John Magufuli alipofika pale Himo alikuja mpaka kwangu na kunisalimia mimi na mke wangu, tangu hapo hawa jamaa wengine walinishambulia kama mpira wa kona,”alisema Mrema huku akishangiliwa ukumbi mzima.

Mwenyekiti wa UDP, John Cheyo  alisema vyama vya upinzani haviwezi kuking’oa CCM kwa kuwa ni chama kigumu.