Magufuli amteua Massawe kuwa Kaimu Mkurugenzi NIDA

Rais John Magufuli

Muktasari:

Taarifa iliyoletwa na Kitengo cha Habari cha Ikulu inaeleza kuwa kabla ya uteuzi huo Massawe alikuwa Mkurugenzi wa Mifumo ya Kompyuta katika Benki Kuu Tanzania (BOT).

Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli leo  amemteua  Andrew Wilson Massawe kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).

Taarifa iliyoletwa na Kitengo cha Habari cha Ikulu inaeleza kuwa kabla ya uteuzi huo Massawe alikuwa Mkurugenzi wa Mifumo ya Kompyuta katika Benki Kuu Tanzania (BOT).

Andrew Wilson Massawe anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Modestus Francis Kipilimba ambaye jana ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa. Uteuzi wa   Massawe unaanza mara moja.