Redio Magic FM, Five Arusha vyafungiwa

Muktasari:

Nape amesema jana kuwa uamuzi wa kuvifungia vituo hivyo umefikiwa baada ya kujiridhisha kwamba vilirusha matangazo yenye kukiuka kanuni za utangazaji.

Dar es Salaam. Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amevifungia kwa muda vituo vya Redio Five Arusha na Redio Magic FM Dar es Salaam kwa madai ya kurusha matangazo ya uchochezi yanayoweza kuleta uvunjifu wa amani.

Nape amesema jana kuwa uamuzi wa kuvifungia vituo hivyo umefikiwa baada ya kujiridhisha kwamba vilirusha matangazo yenye kukiuka kanuni za utangazaji.

Amesema Agosti 25, saa 2.00 usiku hadi saa 3.00 Redio Five kupitia kipindi chake cha matukio, ilirusha matangazo ya uchochezi.

Kuhusu Redio Magic, Waziri Nape amesema Agosti 17 saa 1.00 hadi 2.00 asubuhi kupitia kipindi cha ‘Morning Magic’ katika kipengele cha ‘kupaka rangi’ kilikuwa na maudhui ya uchochezi unaoweza kuleta uvunjifu wa amani.