Burundi yamwaga msaada waathirika wa tetemeko la ardhi

Muktasari:

Waziri wa Afrika Mashariki wa Burundi, Leontine Nzeyimana akikabidhi msaada huo leo wilayani Ngara amesema msaada ulitolewa  na nchi hiyo ni mchele tani 100, mahindi tani 50, sukari  tani 30 na majani  ya chai tani tatu.

NGARA: Serikali ya Burundi imetoa msaada wa vyakula kwa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera na kuvikabidhi kwa viongozi wa mkoa huo wakiongozwa na  Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Dk Suzan Kolimba aliyeiwakilisha Tanzania

 Waziri wa Afrika Mashariki wa Burundi, Leontine Nzeyimana akikabidhi msaada huo leo wilayani Ngara amesema msaada ulitolewa  na nchi hiyo ni mchele tani 100, mahindi tani 50, sukari  tani 30 na majani  ya chai tani tatu.

 Nzeyimana amesema wakazi wa Kagera waliokumbwa na tetemeko hilo ni ndugu wa wananchi waliko nchini Burundi hivyo nchi imeguswa na na athari hiyo na kwamba msaada huo ni kidogo lakini   upokelewe kwa lengo la kukuza mahusiano na ujirani mwema.