Kamati ya Bunge yainusuru TFC

Muktasari:

Pia, kamati hiyo imebaini kuwa kampuni hiyo licha ya umuhimu wake kwa sekta ya kilimo nchini, haina bodi ya wakurugenzi.

Dodoma. Hatimaye Kamati ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma (PIC), imechukua hatua za kuinusuru Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC) inayokabiliwa na hali mbaya kutokana na kupata hasara ya Sh30.2 bilioni mwaka jana.

Pia, kamati hiyo imebaini kuwa kampuni hiyo licha ya umuhimu wake kwa sekta ya kilimo nchini, haina bodi ya wakurugenzi. Kufuatia hali hiyo, kamati hiyo ilishindwa kujadili taarifa ya  Mthibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka 2014/15 ya kampuni hiyo, hivyo kuipangia tarehe nyingine.

Makamu Mwenyekiti wa PIC, Lolencia Bukwimba amesema kamati hiyo  imeshindwa kujadili ripoti hiyo ya ukaguzi, hivyo kuitaka  TFC irudi Oktoba 28.