‘Muswada wa Sheria ya Huduma ya Vyombo vya Habari unajadilika’

Msemaji wa Serikali Hassan Abbas

Muktasari:

Pia, amesema siku kumi zimeongezwa kwa ajili ya kupokea maoni ya kuboresha muswada huo.

Dar es Salaam. Msemaji wa Serikali Hassan Abbas amesema hoja ya wadau kuhusu madai ya kuongezwa muda ili kujadili na kuboresha Muswada wa Sheria ya Huduma ya Vyombo vya Habari ya 2016, inajadilika.

Pia, amesema siku kumi zimeongezwa kwa ajili ya kupokea maoni ya kuboresha muswada huo.

 Amesema kwa kutumia ushawishi wa nguvu ya hoja, yako mambo yaliyokubaliwa na yaliyokataliwa katika Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Maendeleo ya Jamii.

Kauli hiyo ameitoa wakati wa mahojiano maalumu na Kituo cha Matangazo cha Azam TV, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ratiba yake katika kuzungumzia muswada huo.

Katika mjadala huo, mwakilishi kutoka Baraza la Habari Tanzania(MCT), Pili Mtambalike aliyeonyesha msimamo wa kutofautiana na baadhi ya vipengele, amesema hoja ya kuongezewa muda inalenga kushirikisha wadau wengine kabla ya kupitishwa na Bunge.