JKT yakabidhi madawati 2,148

file photo

Muktasari:

Akikabidhi madawati hayo kwa Mbunge wa Muhambwe wilayani Kibondo mkoani Kigoma, Kaimu Mkuu wa Kikosi cha 824 Kanembwa, Meja Hamis Maulid alisema yametengenezwa kwa gharama ya Sh60.81 milioni.

Kibondo. Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), limetengeneza madawati 2,148 na kuyakabidhi kwenye majimbo manne mkoani Kigoma na Shinyanga.

Akikabidhi madawati hayo kwa Mbunge wa Muhambwe wilayani Kibondo mkoani Kigoma, Kaimu Mkuu wa Kikosi cha 824 Kanembwa, Meja Hamis Maulid alisema yametengenezwa kwa gharama ya Sh60.81 milioni.

Alisema mkoani Kigoma, madawati hayo yatagawanywa kwenye majimbo ya Muhambwe na Buyungu na mengine yatapelekwa Ushetu na Kahama mkoani Shinyanga.