TMA yatabiri mvua yam awe Kanda ya Ziwa

Mkurugenzi mtendaji wa TMA, Agnes Kijazi

Muktasari:

Utabiri huo umeonyesha kuwepo kwa mawingu ng'amba ambayo huambatana na radi kali kisha kusababisha mvua hizo.

Dar es Salaam. Mikoa ya kanda ya ziwa huenda ikaendelea kukumbwa na mvua za mawe katika kipindi cha mwezi Novemba kutokana na utabiri uliofanywa na Mamlaka ya Hali Hewa (TMA).

Utabiri huo umeonyesha kuwepo kwa mawingu ng'amba ambayo huambatana na radi kali kisha kusababisha mvua hizo.

Hayo yamesemwa na mkurugenzi mtendaji wa TMA, Agnes Kijazi leo alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu mwelekeo wa msimu wa mvua za vuli Novemba.

"Tulishuhudia maeneo ya Mtimbwa, Sumbawanga, Rusumo, Ngara mvua za mawe zilinyesha na utabiri wa mwezi huu zinaweza kuendelea kunyesha maeneo hayo," amesema Kijazi