Wednesday, December 28, 2016

Korosho za Sh120 milioni zawatia matataniKorosho

Korosho 

By Mwanja Ibadi, Mwananchi mwananchi@mwananchipapers.co.tz

Lindi. Watu wawili mkoani Lindi wanashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kukutwa wakisafirisha korosho tani 43 zenye thamani  ya Sh120 milioni zinazodaiwa kupatikana kinyume na utaratibu.

 Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi ametoa taarifa hiyo kwenye mkutano na waandishi  wa habari ofisini kwake.

Zambi amesema wakati msimu wa zao hilo unakaribia kuisha, kikosi kazi cha udhibiti wa ununuzi wa korosho kinyume na taratibu kimewakamata watuhumiwa hao wakazi wa Tabata, Dar es Salaam na Masasi, Mtwara.

Amesema watu hao wamekamatwa kwenye kituo cha ukaguzi wa mazao cha Mnazi Mmoja katika Manispaa ya Lindi wakiwa  wanasafirisha tani 43 kwa kutumia vibali bandia.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, Mohamed Liwata amesema wanatarajia kuwafikisha mahakamani watu hao ili sheria ichukue mkondo wake.

Kwa habari zaidi soma gazeti la Mwananchi

-->