Eneo dogo chanzo cha migogoro- Dk Kebwe

Muktasari:

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dk Stephen Kebwe amesema  hayo mwishoni mwa wiki mjini Morogoro wakati akimkaribisha Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi kufungua semina ya waandishi wa habari kuhusu masuala ya upimaji ardhi.

Morogoro. Imeelezwa kuwa chanzo cha migogoro ya wakulima na wafugaji mkoani Morogoro ni uwapo wa mifugo mingi kupita uwezo wa eneo la malisho.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dk Stephen Kebwe amesema  hayo mwishoni mwa wiki mjini Morogoro wakati akimkaribisha Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi kufungua semina ya waandishi wa habari kuhusu masuala ya upimaji ardhi.

Amesema eneo la malisho ni dogo mkoani humo ambalo ni ekari 370,000 zinazopaswa kuwa na ng’ombe 185,000 lakini hadi sasa mkoa huo unakadiriwa kuwa na wanyama hao milioni 1.2.

“Hii ni mbaya sana, ni vurugu tupu,” amesema Dk Kebwe na kuonya kwamba wanaoleta vurugu wawe wakulima au wafugaji, watashughulikiwa ipasavyo kwa kuwa hakuna mtu aliye juu ya sheria.