Sh114.57 bilioni kuboresha huduma ya maji

Muktasari:

Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa anayeshughulikia masuala ya maji, Fredius Magige amesema mwaka huu wa fedha Serikali imetenga Sh2.3 bilioni kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya maji katika miji hiyo kwa kupunguza upotevu ingawa fedha hizo bado hazijatumwa kwao.

Mbeya.  Imeelezwa kuwa Sh114.57 bilioni zinahitajika kuboresha huduma ya maji katika miji ya makao makuu na mji midogo ya wilaya sita mkoani hapa ili kutosheleza mahitaji kwa asilimia 100.

Miji hiyo ni Chunya na Tukuyu, Kyela, Rujewa, Kasumulu  na Mbalizi.

Hayo yameelezwa katika taarifa ya mikakati ya kuboresha huduma za maji iliyotolewa kwenye Kamati ya Ushauri  ya Mkoa (RCC) na nakala yake kupatikana hapa jana.