Tuesday, January 3, 2017

Katibu wa CCM Monduli afariki dunia

 

By Mussa Juma, Mwananchi mjuma@mwananchi.co.tz

Arusha. Katibu wa CCM Wilaya ya Monduli, Jacob Nkomola amefariki dunia katika Hospitali ya Temeke jijini Dar es Salaam.

Nkomola ambaye aliteuliwa kuwa katibu wa chama hicho wilayani humo, Novemba Mosi mwaka jana akitokea Wilaya ya Musoma mkoani Mara, alifariki  dunia jana saa moja asubuhi.

Kaimu Katibu wa CCM Mkoa wa Arusha, Omar Bilal na Katibu Mwenezi na Itikadi wa chama hicho mkoani hapa, Shaban Mdoe  walithibitisha kutokea kifo hicho.

Bilal amesema Nkomola alifikwa na mauti hospitalini hapo alikopelekwa kwa matibabu baada ya kujisikia vibaya saa 10:00 alfajiri akiwa nyumbani kwake Dar es Salaam.

-->