Wednesday, January 4, 2017

Fedha za posho kupelekwa kwenye miradiWaziri Mkuu, Kassim Majaliwa

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa 

By Deogratius Kamagi, Mwananchi dkamagi@mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Hatimaye Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ametangaza kufuta  posho zote ambazo hazipo kwa mujibu wa sheria katika halmashauri zote nchini, badala yake fedha hizo zitapelekwa kwenye miradi ya maendeleo.

Majaliwa amesema hayo jana alipotembelea wilaya mpya ya Kigamboni kukagua miradi ya maendeleo, ambako alitumia fursa hiyo kuzungumza na watumishi.

Akizungumzia posho, Waziri Mkuu alitoa mfano wa halmashauri za Dar es Salaam, kwamba Manispaa ya Kinondoni kwa mwaka jana pekee ilitumia Sh1.5 bilioni ikifuatiwa na Ubungo iliyotumia Sh960 milioni.

“Wilaya ya Ilala walitumia zaidi ya Sh400 milioni, ikifuatiwa na Temeke na Kigamboni ambazo kila moja ilitumia Sh189 milioni kwa ajili ya kulipa posho ambazo hazipo katika utaratibu,” amesema.

-->