Hali ya chakula nchini yazua utata

Muktasari:

Kauli hiyo imekuwa wakati Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe akidai kuwa hali ya chakula nchini siyo nzuri kutokana na uhifadhi mbaya,

Zitto amedai jana kuwa Ghala la Taifa la Chakula (SGR) lina hifadhi ya chakula kinachotosha kwa siku nane tu wakati Novemba 2015 kulikuwa na chakula cha kutosha miezi miwili.

Dar es Salaam. Serikali imesema hali ya chakula ni shwari licha ya baadhi ya maeneo kutopata mvua za wastani.

Kauli hiyo imekuja wakati Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe akidai kuwa hali ya chakula nchini siyo nzuri kutokana na uhifadhi mbaya,

Zitto amedai jana kuwa Ghala la Taifa la Chakula (SGR) lina hifadhi ya chakula kinachotosha kwa siku nane tu wakati Novemba 2015 kulikuwa na chakula cha kutosha miezi miwili.

Kwa mujibu wa Zitto, taarifa ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ya Novemba inaonyesha kuwa Mamlaka ya Taifa ya Hifadhi ya Chakula (NFRA), imebaki na tani 90,476 tu za chakula ambacho amedai ni cha kutosholeza siku nane.

Hata hivyo, Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk Charles Tizeba alijibu madai hayo ya Zitto akisema nchi ina chakula cha kutosha wala siyo cha siku nane wala mwezi pekee, bali zaidi.