Monday, January 9, 2017

Jamii yatakiwa kufuga sungura kwa maendeleo

By Habel Chidawali, Mwananchi hchidawali@mwananchi.co.tz

Dodoma. Wafugaji wa sungura mkoani hapa wameshauriwa kutumia njia zenye tija katika ufugaji ili kuongeza kipato na kutafutiwa soko la uhakika.

Rai hiyo ilitolewa na shirika lisilo la kiserikali la Tanzania Business Creation Company Limited (TBCC) katika mafunzo kwa wafugaji yenye  kauli mbiu ‘Mhudumie sungura akuhudumie kiuchumi.

Mkurugenzi mwenza wa TBCC, Elibariki  Mchau alisema ufugaji wa sungura una faida inayoweza kuwatajirisha wananchi wenye kipato cha chini lakini wengi hawajui umuhimu wake kiuchumi.

Alisema wenyeji wa Dodoma hawana utamaduni wa kufuga sungura na mara nyingi hawaamini kama mpango huo unaweza kuwasaidia.

-->