Azzan aungana na Gwajima, Manji

Mbunge wa zamani wa Kinondoni, Iddy Azzan

Muktasari:

Azzan amewasili kituoni hapo muda wa saa 09:06 kwaajili ya mahojiano na polisi baada ya kutakiwa kufanya hivyo na mkuu wa mkoa.

Dar es Salaam. Mbunge wa zamani wa Kinondoni, Iddy Azzan ameripoti katika kituo kikuu cha polisi kama aliyotakiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Azzan amewasili kituoni hapo muda wa saa 09:06 kwaajili ya mahojiano na polisi baada ya kutakiwa kufanya hivyo na mkuu wa mkoa.

Azzan ni miongoni mwa watu 65 waliotajwa na mkuu wa mkoa juzi kutakiwa kufika polisi jijini Dar es Salaam.

Jana Askofu wa kanisa la ufufuo uzima Josephat Gwajima na mfanyabiashara maarufu, Yusuf Manji ambao nao wapo katika orodha hiyo ya mkuu wa mkoa waliripoti.

Kamanda wa Kanda Maalumu, Simon Sirro amesema atazungumza na waandishi wa habari leo saa saba mchana