Ng’ombe 600 wakamatwa ndani ya hifadhi ya Serengeti

Muktasari:

Akizungumza na waandishi wa habari,mhifadhi mkuu wa hifadhi ya Taifa ya Serengeti, William Mwakilema amesema  ng’ombe hao wamekamatwa jan usiku ndani ya hifadhi hiyo.

Serengeti. Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, inashikilia zaidi ya ng’ombe 600 ambao wamekamatwa wakiwa kwenye malisho ndani ya hifadhi hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari,mhifadhi mkuu wa hifadhi ya Taifa ya Serengeti, William Mwakilema amesema  ng’ombe hao wamekamatwa jan usiku ndani ya hifadhi hiyo.

Mwakilema amesema imekuwa kawaida kwa wafugaji hao, kutoka wilaya zinazopakana na hifadhi hiyo  kuingiza mifugo ndani ya hifadhi usiku wa manane na kuitoa alfajiri.

“Hivi sasa tumeimarisha ulinzi ndio sababu tumeendelea kukamata mifugo inayoingizwa mifugo ndani ya hifadhi,”amesema.