Tizeba azitaka taasisi kuwajengea uwezo wakulima

Muktasari:

Kadhalika Tizeba amezitaka taasisi hizo  kutoa mikopo yenye riba nafuu.

Dar es Salaam.Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi,Dk Charles Tizeba amezitaka taasisi na Mashirika ya Maendeleo ya kilimo nchini, kuwajengea uwezo wakulima ili kuongeza thamani ya mazao.

Kadhalika Tizeba amezitaka taasisi hizo  kutoa mikopo yenye riba nafuu.

Waziri huyo ameyasema hayo leo kwenye WARSHA ya kuhitimisha mradi wa kuwezesha maisha kupitia Maendeleo ya mifugo na kilimo(LEAD),uliofanywa na Shirika la Brac Tanzania.

Mradi huo uliofanyika kwa miaka minne,umewezesha kutoa mafunzo ya kilimo pamoja na uwezeshaji kwa mikopo na masoko na kuwanufaisha watu 105,000 nchini