Wabunge waliosoma kwa mkopo watakiwa kujihakiki

Muktasari:

Hayo yamesemwa bungeni leo Ijumaa na Naibu Spika, Dk tulia Ackson wakati akitoa tangazo kwa wabunge kuhusu mikopo hiyo huku akisisitiza waliosoma kwa mkopo wanatakiwa kulipa kwa kuwa na yeye alifanya na amekwishalipa.

Dododoma. Wabunge waliosoma kwa mikopo ya elimu ya juu wametakiwa kujaza fomu za uhakiki ili kubaini kama wamekamilisha malipo au bado wanadaiwa ili kuepuka usumbufu, kudhalilishwa na hatimaye kufikishwa mahakamani.

Hayo yamesemwa bungeni leo Ijumaa na Naibu Spika, Dk tulia Ackson wakati akitoa tangazo kwa wabunge kuhusu mikopo hiyo huku akisisitiza waliosoma kwa mkopo wanatakiwa kulipa kwa kuwa na yeye alifanya na amekwishalipa.

Amesema wabunge wanaotakiwa kujaza fomu hizo za uhakiki ni wale waliosoma kuanzia mwaka 1994/95.