Rais Magufuli aomba dakika tano apitia ripoti ya mchanga wa madini na kurudi kuizungumzia

Rais John Magufuli 

Muktasari:

Ripoti hiyo imekabidhiwa leo kamati aliyoiunda kuangalia ni kiasi gani cha dhahabu kilichopo kwenye mchanga huo.

Dar es Salaam. Rais John Magufuli ameomba apewe dakika tano kwenda kupitia ripoti ya makontena ya mchanga wa dhahabu kabla hajazungumza kisha kwenda kwa dakika hizo na kurudia kuanza kuzungumzia.

Ripoti hiyo imekabidhiwa leo kamati aliyoiunda kuangalia ni kiasi gani cha dhahabu kilichopo kwenye mchanga huo.

Mwenyekiti wa Kamati ya wajumbe wanane waliochunguza makontena 277 ya mchanga wa dhahabu iliongozwa na Profesa Abdulkarim Mruma.

Kamati hiyo ya wataalamu wa jiolojia na uchambuzi wa kisayansi iliyoundwa Machi 29 mwaka huu, ilichunguza aina ya madini yaliyopo, kiasi na viwango vya ubora.

Akikabidhi ripoti hiyo, Profesa Mruma amesema uchunguzi huo umebaini uwepo wa madini ya kiasi cha kati ya Sh829.4 bilioni mpaka 1.439 Trillion kwa makontena yote 277.

"Licha ya uchunguzi uliofanywa kupitia makontena haya, tumegundua uwepo wa aina nyingi zaidi za madini ambayo hayakuwa yakijulikana na haya yamekutwa na thamani ya kati Sh129.5 bilioni mpaka261 bilioni," amesema Profesa Mruma.