Askofu Gwajima azungumzia sakata la madini

Muktasari:

Akizungumza kwenye ibaada kanisani kwake leo Askofu Gwajima amesema, "Tusiogope kushtakiwa Magufuli(Rais John) piga marufuku makinikia kusafirishwa nje." 

Dar es Salaa,. Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amesema ni muhimu madini yasichimbwe hadi itakapowekwa mashine za kuchenjua makinikia.                       

Akizungumza kwenye ibaada kanisani kwake leo Askofu Gwajima amesema, "Tusiogope kushtakiwa Magufuli(Rais John) piga marufuku makinikia kusafirishwa nje."                       

"Madini yaliyopo Tanzania ni zaidi ya 300 lakini bado tuna umaskini tumelogwa na nani."