Asasi 153 za kiraia zapatiwa ruzuku

Muktasari:

Kati ya asasi za kiraia 632 zilizoomba, 153 ndizo zilizopewa fedha ambako asasi hizo zimehimizwa kufanya matumizi sahihi.

Dodoma. Shirika la Foundation for Civil Society limetoa ruzuku ya Sh10.1 bilioni kwa asasi za kiraia 153 nchini.

Fedha hizo ni kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali nchini kwa mwaka huu.

Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo, Francis Kiwanga amesema leo, Julai 26 kuwa kati ya asasi za kiraia 632 zilizoomba kupatiwa ruzuku, zilizopata ni 153.

"Napenda kuwakumbusha kufanya matumizi sahihi ya ruzuku mtakazopewa. Tunafahamu kuwa taasisi inawajibika kwa wananchi na kwa wafadhili, kwa mantiki hiyo The Foundation hatutarajii kwa namna yoyote kuona matumizi yanakuwa kinyume cha utaratibu," amesema.