Lissu anyimwa dhamana

Muktasari:

  • Mwanasheria huyo wa Chadema anafikishwa mahakamani kesho

 Mwanasheria wa Chadema na Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu amenyimwa dhamana baada ya kukamatwa leo kwa tuhuma za kumkashifu Rais John  Magufuli na uchochezi.

Akizungumza na Mwananchi leo  mwanasheria wake Faraji Mangula amesema kwamba kesho Lissu atapandishwa mahakamani.

Amesema Polisi wamedai kwamba amemkashifu Rais a wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari  kwenye hoteli ya Protea.

‘’Polisi wamemnyima dhamana wamesema wanafanya utaratibu wakumfikisha mahakamani’’amesema.