Madiwani wafunga barabara Geita

Muktasari:

Kwa ufupi

Wafanyakazi wa mgodi huo wametakiwa wasifike kazini kutokana na mgogoro uliopo mpaka watakapotangaziwa.

Madiwani na wananchi wilaya ya  Geita wamefunga barabara inayoingia mgodini kuzuia magari ya mgodi yasiingie hadi mgodi wa GGM mpaka walipe kodi Dola   12milioni wanazodaiwa.

Madiwani wa halmashauri mbili za wilaya ya  Geita wamezuia magari ya mgodi kuingia au kutoka mgodini hadi watakapolipa kodi ya huduma wanayodai kuanzia mwaka 2003 hadi 2013

Ofisa uhusiano  Mgodi  huo  Manase Ndoroma amesema  wao wamelipa kihalali kwa mujibu wa sheria  na kwamba kilichotokea ni migongano ya kisheria ambazo zote zimetungwa na bunge.

Polisi wameimarisha ulinzi katika maeneo ya Nungwe uliko mradi wa maji unaosambaza maji mgodini ,eneo la uwanja Wa Ndege na geti la kuingia mgodini ambako kote kuna askari wenye silaha.