Familia ya Babu Seya yaibukia Mapinduzi Zanzibar

Dar es Salaam. Familia ya mwanamuziki  Nguza Vicking 'Babu Seya' leo Ijumaa imeungana na Wazanzibari kwa ajili ya kusherehekea maadhimisho ya miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

 

Maadhimisho hayo yaliyafanyika leo Ijumaa katika Uwanja wa Amaan Zanzibar yakihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa akiwamo Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein.

Tayari Serikali imewatafutia studio ya kurekodi muziki familia familia hiyo baada ya kuonana na Rais John  Magufuli  Ikulu waliopokwenda kutoa shukurani. 

Mmoja mtoto wa Babu Seya, Michael Nguza maarufu kama Nabii Nguza aliliambia Mwananchi kuwa lengo la kwenda Zanzibar ni kusherekea maadhimisho ya mapinduzi hayo.

“Tumekuja kusherehekea  sikukuu ya Mapinduzi ya Zanzibar,” amesema Nabii Nguza.

 

Babu Seya na wanawe Johnson Nguza ‘ Papii Kocha na Nabii Nguza wameanza kuonekana hadharani mfululizo ikiwa ni baada ya kuonana na Rais Magufuli walikokwenda kutoa shukurani baada ya kuachiwa huru Desemba 9 mwaka jana.

Baada ya kuonana na Rais Magufuli siku zilizofuata wakiwa na , Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni,  Sanaa na Michezo, Juliana Shonza walikwenda  katika Studio  za Wanene zilizopo Mwenge  kwa ajili ya mchakato wa kuanza kufanya kazi zao.