Wasanii wagawana majukumu msiba wa Masogange

Muktasari:

Kamati ya awali iliyoundwa imemchangua Mchopanga kuwa katibu na Zamaradi kukusanya michango.

Dar es Salaam. Wasanii mbalimbali wa filamu na wa bongo fleva, wamekutana katika viwanja vya Leaders Club jioni hii ili kujadiliana kuhusu utaratibu wa mazishi ya msanii anayepamba video za muziki (video queen), Agness Gerald maarufu Masogange.

 

Steve Nyerere ameiambia MCL Digital kuwa, Masogange anatarajiwa kuzikwa Mbeya na kuwa mwili utasafirishwa Jumapili wiki hii na kuzikwa Jumatatu.

 

Miongoni mwa wasanii waliofika Leaders leo ni pamoja na Chopa wa Mchopanga, Irene Uwoya aliyeambatana na mume wake, Dogo Janja na aliyekuwa mtangazaji wa Clouds Media Group, Zamaradi Mketema.

 

Kamati ya awali iliyoundwa, imemchangua Mchopanga kuwa katibu na Zamaradi kukusanya michango.

 

“Lakini tukipata taarifa kutoka kwa ndugu tutajua msiba utagharimu shilingi ngapi kwa sasa mahitaji makubwa ni mabasi mawili kwa ajili ya kusafirisha mwili, maturubai, vyakula na maji,” amesema Nyerere.