VIDEO-Masogange asindikizwa na wimbo wa Masogange

Muktasari:

  • Wimbo huo unapigwa kwenye msiba wa Masogange huku watu wakilia na wengine kuucheza

Mbeya. Mwili wa msanii Agnes Gerald ‘Masogange’ tayari umewasili Utengule, mjini Mbeya, huku wimbo unaotumika katika maombelezo wa msiba huo ukiwa ni ule wa msanii Abelnego Damian ‘Belle 9’ uitwao  Masogange.

Wimbo huo uliotoka mwaka 2011, ndio uliompandisha chati marehemu na kujikuta anaitwa Masogange hadi hii leo.

Mwili wa Masogange uliwasili majira ya saa tano asubuhi na kupokelewa na makada wa Chama cha Mapinduzi(CCM) waliokuwa wamevalia sare za chama hicho na kuingizwa moja kwa moja ndani ya nyumba ya baba yake aliyokuwa amemaliza kumjengea siku za hivi karibuni.

Kupigwa kwa wimbo huo kuliibua simanzi kwa waombolezaji waliofika katika msiba huo japokuwa wapo wengine waliokuwa wakiucheza.

Wasanii wameshindwa kujizuia na kuangua vilio.