Kichaa cha mbwa tishio Iringa Mjini, dawa zahitajika

Muktasari:

Rweymamu alisema kwa mwaka wilaya hiyo hupata wagonjwa 100 hadi 120 wanaotumia chupa 350, lakinimahitaji halisi ni chupa 500.

Iringa. Wilaya ya Iringa Mjini ina uhitaji chupa 500 za dawa ya kutibu kichaa cha mbwa kutokana na kuwapo kwa idadi kubwa ya wagonjwa. Hayo yalisemwa jana na mfamasia mkuu wa wilaya hiyo, Deogratius Rweymamu alipokuwa akitoa taarifa kwa wanahabari kuhusu hali ya upatikanaji dawa zinazosambazwa moja kwa moja na Bohari ya Dawa (MSD).

Rweymamu alisema kwa mwaka wilaya hiyo hupata wagonjwa 100 hadi 120 wanaotumia chupa 350, lakinimahitaji halisi ni chupa 500.

“Kwa mfano mwezi mmoja uliopita tuliagiza chupa 240, lakini tukapewa 120,” alisema.

Naye kaimu mganga mkuu wa Kituo cha Afya Inyala wilayani Mbeya Vijijini, Alvin Mutiganzi alisema changamoto wanayokabiliana nayo ni baadhi ya waathirika wa Ukimwi kugoma kuanza dawa mapema.