Serikali yaondoa VAT kwenye taulo za kike

Viongozi mbalimbali kutoka serikalini, vyombo vya ulinzi na usalama na taasisi mbalimbali wakisoma vitabu vya hotuba ya Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2018/2019, ilipokuwa ikiwasilisha bungeni na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango, jijini Dodoma leo. Picha na Edwin Mjwahuzi

Muktasari:

Bunge lililipuka kwa shangwe na vigelegele 

Dodoma. Serikali imefuta Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT),  kwa taulo za kike (pedi) zinazoagizwa kutoka nje ya nchi.

Msamaha huo umetangazwa leo Alhamisi Juni 14 na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango alipokuwa akiwasilisha bajeti  kuu ya serikali kwa mwaka 2018/19.                                                                                        “Napendekeza kusamehe VAT kwenye taulo za kike kwa lengo la kuwezesha upatikanaji wa bidhaa hizo kwa bei nafuu kulinda afya ya mama na mtoto wa kike hasa walio vijijini na shuleni,” amesema waziri.

Baada ya kutangaza msamaha huo, Bunge lililipuka kwa shangwe na vigelegele ikizingatiwa ni suala lililokuwa na mchango mkubwa wakati wa mijadala ya hoja za wizara mbalimbali zilizwasilishwa kwenye vikao vinavyoendelea. Hali hiyo ilimfanya pia, Spika Job Ndugai kumuomba Waziri Mpango arudie kipande hicho na akarudia.

Endelea kutufuatilia