Dk Shein ateua mrithi wa Jecha ZEC

Muktasari:

  • Pia ameteua wajumbe sita wa tume hiyo

Dar es Salaam. Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein amemteua Jaji Mkuu mstaafu wa Zanzibar, Hamid Mahmoud Hamid kuwa mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC).

Taarifa iliyotolewa leo Juni 20, 2018 na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Dk Abdulhamid Yahya Mzee imesema Dk Shein pia ameteua wajumbe sita wa tume hiyo.

Wajumbe walioteuliwa ni Mabruki Jabu Makame, Feteh Saad Mgeni, Makame Juma Pandu, Dk Kombo Khamis Hassan, Jaji Khamis Ramadhan Abdulla na Jokha Khamis Makame.

Taarifa hiyo inabainisha kuwa uteuzi huo umeanza leo, huku wajumbe hao wakitakiwa kufika Ikulu Ijumaa Juni 22, 2018 kwa ajili ya kuapishwa.

Kabla ya uteuzi huo, Jecha Salim Jecha ndio alikuwa mwenyekiti wa ZEC.