Maonyesho ya Sabasaba yaanza kunoga

Baadhi ya gari zilizowasili Leo kutoka kampuni ya GF zikiwa zimeengeshwa ndani ya banda LA Kampuni hiyo katika viwanja vya maonyesho vya Mwalimu Julius Nyerere tayari kwaajiri ya maonyesho ya Sabasaba yanyotaraji kuanza  2 8Juni had I 13Julai.Picha na Jackline Masinde

Muktasari:

  • Wafanyabiashara waanza kuingiza bidhaa zao

Dar es Salaam. Baadhi ya wafanyabiashara wameanza kuingiza bidhaa zao katika viwanja yanapofanyika maonyesho ya 42 ya kimataifa ya biashara Dar es Salaam maarufu kama Sabasaba.

Maonyesho hayo yataanza Juni 28 hadi Julai 13, 2018 huku nchi 32 na wafanyabiashara zaidi ya 2,000 wakitarajiwa kushiriki.

Leo Jumapili Juni 24, 2018 MCL Digital imefika katika viwanja hivyo vilivyopo wilayani Temeke na kuwashuhudia wafanyabiashara hao wakianza kupanga bidhaa katika mabanda, wengine kuanza kwa kuyasafisha.

Ofisa Uhusiano wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tantrade), Theresa Chilambo alisema mbali na wafanyabiashara kuanza kuingiza bidhaa zao, wengi wao kwa sasa wameanza kwa kukarabati mabanda yao.