VIDEO: 14 waliofariki dunia ajali ya Mkuranga watajwa

Muktasari:

Ajali hiyo iliyohusisha basi dogo la abiria na lori la mchanga imetokea leo alfajiri katika eneo la Dundani wilayani Mkuranga Mkoa wa Pwani


Mkuranga. Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Mkuranga Steven Mwandambo ametaja majina ya waliofariki dunia katika ajali  iliyohusisha basi dogo aina ya Toyota Hiace lililobeba wanafamilia na lori la mchanga iliyotokea leo alfajiri Juni 25, 2018  eneo la Dundani wilayani Mkuranga Mkoa wa Pwani.

Akizungumza na MCL Digital leo Mwandambo amesema wamepokea miili ya watu 14 na majeruhi wanne, kwamba watatu wamehamishiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa ajili ya matibabu zaidi,”majeruhi mmoja amebaki Mkuranga anaendelea vizuri.”

Amesema kati ya waliofariki, wanawake  ni saba  na wanaume saba, akiwemo mtoto wa miaka mitatu.

Waliofariki dunia katika ajali hiyo ni Watende Chanzi, Mwanaisha Chanzi,  Sikujua Chanzi,  Omari Chanzi,  Ally Chanzi, Ally Kilumanda, Sharifa Kilumanda.

Wengine Selemani Jaka, Hassan Kibendera, Zuhura Lipipi, Sauda Mbigili, Haji Mtonda, Ashura Hassan na Rashid Hassan.

Amesema majeruhi ni  Nuldini Mohamed, Islamu Nuldini, Sabra Salum na Mohamed Ally.

“Miongoni mwa majeruhi mmoja hali yake ni mbaya na madaktari wanapambana kuokoa maisha yake,” amesema.

Akizungumzia ajali hiyo Kamanda wa Kikosi cha Polisi wa Usalama Barabarani nchini, Fortunatus Muslim amesema sababu ya ajali hiyo ni mwendo kasi wa lori hilo.

Amesema lilikuwa katika mwendo kasi, dereva kushindwa kulidhibiti jambo lililosababisha lori hilo kuhamia upande wa kulia wa barabara na kuligonga basi hilo dogo uso kwa uso