Mbunge adaiwa cheti cha ndoa hotelini

Catherine Waruguru 

Muktasari:

Hoteli hiyo imeweka masharti kwamba mwanamume na mwanamke hawawezi kuruhusiwa kuingia  chumba kimoja ikiwa  hawajaoana.


Kericho,Kenya.Mbunge wa jimbo la Laikipia nchini Kenya amelalamika kuzuiwa kuingia hotelini yeye na mume wake baada ya kukosa cheti cha ndoa.

Mbunge huyo  Catherine Waruguru anasema haki zake za kimsingi zimekiukwa  na kutishia kuishtaki hoteli hiyo ya mjini Kericho, eneo la Bonde la Ufa akisema alidhalilishwa.

Hoteli hiyo imeweka masharti  kwamba mwanamume na mwanamke hawawezi kuruhusiwa kuingia  chumba kimoja ikiwa  hawajaoana.

Lakini mbunge huyo anasema wanandoa wengine waliruhusiwa kuingia bila kuulizwa  cheti cha ndoa, na kwamba walifanya kila juhudi kuthibitisha kwamba walikuwa mume na mke ingawa hawakuwa na cheti cha ndoa.