Wema akutwa na hatia, ahukumiwa kifungo cha mwaka mmoja au faini

Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemhukumu msanii wa filamu nchini Wema Sepetu, kulipa faini ya Sh1 milioni kwa kila kosa au kwenda jela mwaka mmoja baada ya kupatikana na hatia ya kutumia na kukutwa na dawa za kulevya aina bangi.

Hukumu hiyo imetolewa leo, Julai 20, 2018 na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Thomas Simba baada ya kumtia hatiani kama alivyoshtakiwa.

Pia mahakama hiyo imewaachia  huru mshtakiwa wa pili na watatu, katika kesi hiyo, ambao ni wafanyakazi wa Wema, Angelina Msigwa na Matirda Abas.