Makamba: Sikukamatwa na polisi, niliwapa maelezo

Muktasari:

  • Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), January Makamba ametoa ufafanuzi kuhusu madai ya kuhojiwa na polisi kuhusu suala la mfanyabiashara Mohammed Dewji ‘Mo’, akibainisha kuwa hakukamatwa kama inavyodaiwa katika baadhi ya mitandao ya kijamii

Dar es Salaam. Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira),  January Makamba ametoa ufafanuzi juu ya taarifa kuwa alikamatwa na polisi kuhusu suala la mfanyabiashara Mohammed Dewji ‘Mo’.

Ametoa ufafanuzi huo kupitia mtandao wa Twitter leo baada ya kusambaa kwa taarifa kuwa alikamatwa.

Hata hivyo, leo Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa  ameithibitishia MCL Digital kuwa jana usiku polisi walichukua maelezo ya  waziri huyo kuhusu suala la Mo.

Katika Twitter Makamba ameandika, “Polisi walinipigia simu  kuniomba kama rafiki wa Mo niwasaidie kama kuna chochote cha ziada ambacho Mo aliniambia kinachoweza kusaidia uchunguzi.”

“Niliwaeleza wakasema kinafanana na alichowaleza (Mo). Wakanishukuru na wamefanya hivi pia kwa wanafamilia (ya Mo). Sikukamatwa.”

Mo alitekwa Oktoba 11 katika Hoteli ya Colosseum alikokwenda kwa ajili ya kufanya mazoezi na kupatikana Oktoba 20 saa 8:00 usiku, baada ya waliomteka kumtelekeza katika viwanja vya Gymkhana, jijini Dar es Salaam.

Makamba ni miongoni mwa watu waliopata taarifa mapema za kupatikana kwa bilionea huyo na kuandika katika mtandao wa kijamii wa Twitter.

Katika ukurasa wa Twitter Makamba aliandika: “Mohammed Dewji amerudi nyumbani salama. Nimezungumza naye kwa simu dakika 30 zilizopita. Sauti yake inaonyesha mzima bukheri wa afya. Shukrani kwa wote kwa dua na sala. Naenda nyumbani kwake kumuona muda huu.